HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 11 May 2018

OFISA MAUZO KAMPUNI YA AGGREY &CLIPFORD KORTINI KWA TUHUMA ZA TAARIFA ZA UCHOCHEZI KUPITIA MTANDAO

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
OFISA Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clipford, Razack Hamad (26) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kijubu shtaka  la kuchapisha taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram.
Razack ambaye ni mkazi wa Mbezi Juu jijini Dar es Salaam amesomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi, Martha Mpazi.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Razack anakabiliwa na shtaka moja  la kuchapisha taarifa ya uchochezi kinyume na kifungu cha 53(1)(c) na 52(1)(a) cha sheria ya habari namba 12 ya mwaka 2016.

Akisomewa shtaka lake imedaiwa,  Machi 9 mwaka huu mshtakiwa Razack akiwa jijini Dar es Salaam alitumia mfumo wa kompyuta katika simu yake kupitia mtandao wake wa Telegram kwa kuandika;

"Nimepata wazo kwa group jingine huko tunaweza kukwepa garama pia kuandika hata kwenye kuta za wazi #April 26 Magufuli Out, pinga Dictator" Maneno ambayo yangeibua chuki kwa Watanzania.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini 2 watakaosani bondi ya Sh.milioni 5.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clipford, Razack Hamad (aliyevaa sweta) akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa shtaka  la kuchapisha taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram nyuma akisindikizwa na askari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad