HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 11 May 2018

MSHANA AILEZA MAHAKAMA ALIVYOSHTUKA ALIPOPOKEA TAARIFA YA BV1 ILIYODAI TBC IMEWASABABISHIA HASARA

*Ni katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana  ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, alishtuka alipopokea taarifa ya usuluhishi(notice of arbitration) kutoka Channel 2 Group Corporation (BV1) iliyopo Uingereza wakidai TBC imewasababishia hasara.

Mshana amedai taarifa hiyo ilimshtua kwa kuwa waliwaahidi kuwapatia kazi ya kuhamisha urushaji wa matangazo ya televisheni  kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali.

leo, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi watatu wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Tido

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

Akizungumza na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, Mshana amedai kuwa, Mei 28 mwaka 2012 walipokea madai ya usuluhishi (Notice of arbitration) yanayohusisha kampuni kudaiwa  pesa nyingi na walipewa siku 28 ty lazima TBC iwe imejibu madai hayo.

Alidai aliwasiliana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TBC kuuliza kama wanajua juu ya taarifa hiyo au kama waliwahi kupitisha suala hilo lakini naye alionekana hakufahamu mkataba huo  ulioingiwa na Tido na  Channel 2 Group Corporation (BV1) .

Mshana aliendelea kudai Mwenyekiti wa bodi alielekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo aandikiwe barua pengine analifahamu suala hilo la mkataba ambapo alidai kuwa Wizara hiyo ya Habari ilimwandikia mwanasheria wa Serikali  (AG) kuliangalia hilo suala na kutoa ushauri wa kisheria na maelekezo.

"Nakumbuka Wizara ikitoa maelekezo kwa bodi ya wakurugenzi ya TBC  iitishe kikao na kujali na kutoa mapendekezo na kwamba Wizara ilitaka kujua zaidi huo mkataba,"amedai.

Alidai kuwa kulikuwepo na Mawasiliano kati ya TBC, Mwanasheria Mkuu(AG) na Wizara kwa sababu unapotakiwa kuingia mkataba ni lazima ipate ridhaa ya AG. Alidai kuwa Msajili wa Hazina naye alifahamishwa kwa sababu yeye ndiyo amepewa dhamana na mali ya shirika pamoja na Wizara ya fedha ambayo ni mtoa fedha.
Aliendelea kutoa ushahidi Katika kesi huyo Mshana alidai kuwa AG aliagiza ateuliwe mwanasheria aliyepo nchini Uingereza kusimamia suala hilo la usuluhishi kwa niaba ya Serikali na ikateuliwa kampuni ya uwakili ya Freshfield Bruckhaus Derringer us  LLP .
Kampuni hiyo gharama zao zilikuwa zikilipwa kwa muda ambapo walilipwa zaidi ya Sh 887 milioni.
Alibainisha kuwa kutokana na mchakato huo TBC ilipata hasara kwa kulazimika kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kampuni hiyo ya uwakili walioitetea TBC fedha ambayo ingeweza kutumika katika kuleta maendeleo mengine
Kwani imewasababishia kukosa faida ambayo wangeipata iwapo wangewekeza katika kuhamisha urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka mfumo wa analojia kwenda digital.

Kesi imeahirishwa hadi Mei 18,2018. Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali  hasara ya ya 887,122,219.19.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad