KAMPUNI ya
Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa zawadi
kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi
hizo Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix Awino amesema Star Times
inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi kupata chakula cha jioni na
malazi ya Hotel ya kisasa.
“tunafurahi
kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama sehemu ya
upendo wetu kwao kwa kuwapa promotion na maudhui yanayoendana na wakati hivyo
kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata malazi SeaScape, Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika ,
Mbeya wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata kupumzika
katika Hotel ya Morena”amesema Awino.
Kwa upande
wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na Startimes, Nuezy
Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja wa Star Times kupata
nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama hiyo hili waweze kufurahi na
wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi cha Star Times.
Amesema kuwa
star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na
kufurahia vipindi bomba vya kila siku.
Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
Bwana na Bibi Alex wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi kampuni ya Star Times Tanzania
Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick
Wafanyakazi wa Star Times Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wameshika maua
Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni Valentine's na Star Times
Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment