Kushoto ni Mama Eda Kapange akikata keki katika hafla hiyo ya
kumuaga, keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga.
Watumishi wa afya wamekumbushwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia
maadili ya taaluma ya kazi ili kuendelea kutoa huduma bora .
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi
na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa alipokua
akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda
Kapange aliyekua akihudumu katika Idara ya watoto Hospitalini hapo.
Amesisitiza kuwa suala la kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ni muhimu kwani
mgonjwa anahitaji upendo na kupewa maneno yenye matumaini na kwamba
hiyo pekee ni tiba .
Pia Mkurugenzi Mtawa amemuelezea Mama Eda Kapange kuwa ni mtumishi
hodari na mchapakazi hivyo amewataka watumishi wengine kuiga mfano
wake kwa vitendo.
Baadhi
ya wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wakimtakia heri na afya njema mama Eda
Kapange katika maisha yake baada ya kulitumikia taifa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa
akitoa neno katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda
Kapange iliyofanyika katika Hosppitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto
wakishangilia huku wakiinua maua juu kama ishara ya upendo.
No comments:
Post a Comment