HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 16, 2013

Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yafana jijini Dar leo

Kikundi cha Watoto wa Asasi ya Tumaini Post Test kutoka Ukonga, Magereza wakiwa tayari kuanza Maandamano leo ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika kuelekea Viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe jijini Dar es Salam.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando(aliyeko katikati) akiwa amesimama kupokea Maandamano ya Watoto leo hawapo pichani katika Kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo katika Kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Sanaa cha Watoto kutoka Manispaa ya Temeke, Mkoani Dar es Salaam wakicheza ngoma ya asili leo mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando hayupo pichani katika Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja Vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watoto ambao wameshiriki Maandamano katika Kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika wakiwa wameketi katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando hayupo pichani.
Sehemu ya baadhi ya Wazazi ambao wamehudhuria katika Kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad