Mshambuliaji wa timu ya Chelsea,Fernando Torres akishangilia goli lake kwa hisia kali sana aliloipachikia timu yake dhidi ya Timu ya Barcelona katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la UEFA.kwa mche zo huu wa leo uliomalizika kwa suluhu ya bao 2 - 2,na kuifanya timu ya Chelsea kutinga hatua ya fainali.kiukweli mchezo huo ulinoga sana na ulikuwa ni wa kuvutia sana (japo kuwa ndugu zetu wa darajani walipaki bonge la lori langoni kwao ambalo lilikuwa likizuia mipira yote ya Barcelona).
Wachezaji wa timu ya Chelsea wakishangilia goli zuri lililofungwa mBrazil,Ramires (pili kulia) wakati wa mchezo wao uliomalizika muda mfupi uliopita dhidi ya timu ya Barcelona.timu hizo zimefungana Bao 2 - 2,lakini kutokana na bao 1 waliloshinda Chelsea katika mchezo uliopita limefanya matokeo kuwa Barcelona 2 - 3 Chelsea na kuifanya timu hiyo kutinga fainali bila ya kuwa na pingamizi lolote.
No comments:
Post a Comment