HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 25, 2012

Japhet Kaseba kuzichapa tena na Francis Cheka

Bondia Japhert Kaseba (kulia) akimwaga wino kwenye katarasi ya mkataba wa kucheza na Francis Cheka siku ya sabasaba,jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mdau Khalifa Kiumbemoto.

Na Mwandishi Wetu

BINGWA wa kick Boxing nchini, Japhet  Kaseba leo amesaini mkataba wa kucheza na Bingwa wa dunia wa ndondi mwenye mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonyesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano

"Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini awajui mimi ni bingwa katika mapigano yote" alisema Kaseba

Kaseba aliendelea kusema "Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za cheka ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa cheka kanikimbia muda mrefu tu tangia tupambane 3 October 2009  ambapo alipewa ubingwa kwa kusingizia mshabiki wangu alikuja kumtupa nje ya uwanja kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika"

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi

Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad