Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akipata taarifa kutoka kwa Askari wa upelezi Peter James Kilalo (38) aliebahatika kujishindia kiasi cha shilingi milioni kumi mara baada ya droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-pesa kuchezeshwa katika Makao makuu ya kampuni hiyo jijijni.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kuchezesha droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-pesa ili kupata mshindi wa shilingi Milioni kumi, wa pili kulia ni Afisa Masoko wa M-pesa Reenu Verma, na Meneja wa Mifumo ya kompyuta Bw. Patrick Makungu pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania bi. Chiku Saleh.
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Kompyuta kutoka kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania bw. Josephat Kyando akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Rukia Mtingwa wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-pesa ili kupata mshindi wa shilingi milioni kumi.
No comments:
Post a Comment