HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 24, 2012

BODI YA TASAF YAKAGUA MIRADI ILIYO CHINI YA UDHAMINI WAKE KISIWANI PEMBA

Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya Ofisi ya Rais (TASAF) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro akiangalia mizinga ya kisasa ya kufugia nyuki ambayo TASAF imetoa msaada kwa wana nchi wakisiwa cha Pemba kuweza kuzalisha asali na kujipatia fedha ilikujikwamua na matatizo ya kiuchumi.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya Ofisi ya Rais (TASAF) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro (alieinama) akiangalia chumvi inayo zalishwa na Wanakikundi wa Shehia ya Chambani kisiwani Pemba ikiwa ni ziara ya TASAF kukagua miradi iliyo chini ya udhamini wake.Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho,Bw. Nassor Suleman.
Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya Ofisi ya Rais (TASAF) wakikagua mradi wa ujenzi wa mlango wa kuzuia maji ya bahari ambayo yalikuwa yana haribu mashamba ya mpunga katika bonde la ukele Kisiwani Pemba,mradi huo wa ujenzi unafadhiliwa na TASAF pamoja na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.
Wapiga picha wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Leah Mushi (kulia) na Mariam Shaban Mtwana wa Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC) wakiwajibika wakati Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya Ofisi ya Rais (TASAF) wakikukagua miradi iliyo chini ya udhamini wake kisiwani Pemba.
Mwenyekiti wa Mradi wa Maji katika Shehia ya Njuguni kisiwani Pemba,Bw. Abdalla Rubea Othman (mwenye kanzu) akimshuru  Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya Ofisi ya Rais (TASAF) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro kutokana na TASAF kusaidia kujenga kisima cha maji katika eneo hilo ambapo siku za nyuma palikuwa na tatizo la maji.Picha na Christopher Mfinanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad