Jumuiya ya watanzania nchini Ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha Mtanzania mwenzetu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI)kilichotokea hospitali ya Nikeas Piraeus J'mosi 18/2/2012.
Marehemu kabla ya kuwasili ugiriki alikuwa ni mkaazi wa Kikwajuni Zanzibar. Hivi sasa tupo katika harakati za michango ya kutuwezesha kumsafirisha nyumbani.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
KATIBU MKUU
Jumuiya ya watanzania Ugiriki
No comments:
Post a Comment