HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2012

shule za kata kukabiliwa na walimu wenye sifa

Na Mery Ayo,Arusha

Shule za kata katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa kanda ya kaskazini zinakabiliwa na changamoto ya walimu wenye sifa za ufundishaji hali ambayo inachangia kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi katika shule hizo.

Mkaguzi wa shule kwa kanda ya kaskazini magharibi bw Victa Bwindiki aliyasema hayo wakati alipokuwa katika mahafali ya saba ya kidato cha sita yaliyofanyka katika shule ya arusha Modern.

Alisema kuwa shule hizo za kata mara nyingi zinapata walimu ambao hawana sifa zinazostahili hali ambayo inaibua changamoto mbali mbali katika shule hizo hivyo kufanya kurudi nyuma kitaaluma

Aliongeza kuwa walimu wa shule za kata wanatakiwa wawe na elimu ya juu sana kwa kuwa shule zote za kata zinakuwa na wanafunzi wengi hivyo ni vema wadau wa elimu wakaweka mikakati ambyo itaweza kupounguza tatizo hilo.

Vile vile alieleza kuwa mbali na tatizo hilo pia shule hizo zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia haswa swala zima la vitabu kwani kitabu kimoja kinalazimika kutumiwa na wanafunzi ishirini hali ambayo inachangia kushuka kwa kiwango cha elimu.

Alisema kuwa kutokana na upungufu huo wa vitabu wanafunzi hushindwa kusoma vitabu kwa kujiamini hivyo amewaomba wazazi pamoja na wadau wote wa elimu kuhakikisha kuwa wanatoa fursa kwa shule za kata kupewa vitabu na kuhakikisha kuwa walimu wenye sifa wanapatikana.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo bw Philip Wasike alisema kuwa nao wakuu wa shule wanatakiwa kujiweka utaratibu maalum wa kuwapa motisha walimu kila mara ili waweze kuongeza bidii katika ufundishaji wao.

Alisema kluwa endapo walimu watapewa motisha kila mara basi ni wazi kuwa watafundisha kwa moyo bila kujali changamoto za mazingira ambayo yanaw3akabili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad