HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2012

Rais Kikwete akabidhi kifuta machozi cha ng'ombe longido, azindua mradi wa uwezeshaji mifugo

Rais Dr.Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Longido wakati wa hafla ya kugawa ng’ombe zaidi ya 25,000 na mbuzi zaidi ya 15,000 kwa kaya zilizoathirika kwa ukame wilayani Longido jumapili.
Mwanafunzi Godlisten Ole Olais anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Longido akiteta jambo na Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 zilizofanyika wilayani longido jumapili.
Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
Mmoja wa Wazee wa Kimasai akimuombea dua Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wilayani Longido Jumapili.
Mzee wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido,Ngorongoro naMonduli.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Longido ngombe watano na mbuzi katika sherehe ambayo jumla ya kaya 16 zilikabidhiwa ngombe na mbuzi baadaya kuathirika na janga la kiangazi ambapo baadhi wakazi wa wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli walipoteza mifugo yao yote.Katika zoezi hilo serikali imetoa jumla ya ngombe zaidi ya 25,000 na zaidi ya mbuzi 15,000 ili kuzisaidia familia hizo kuanza tena maisha yao yanayotegemea sana mifugo.Sherehe za makabidhiano hayo zimefanyika wilayani Longido, mkoani Arusha. 
Morani wa kimasai wakicheza ngoma maalumu wakati wa sherehe hizo.Picha na  mdau Freddy maro wa Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad