Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira mjini Sumbawanga, wakati akimalizia ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkewe Mama Asha Bilal (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkewe Mama Asha Bilal (kushoto kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya (kulia kwake) na baadhi ya viongozi wa mji wa Sumbawanga, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa kampuni za kufanya usafi katika mitaa ya mjini Sumbawanga, wakati akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara kwa ajili ya kudumisha usafi wa mazingira, ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Soko la Tunduma lililofanyiwa ukarabati baada ya kuungua moto mwaka jana, wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya jana. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma jana, kwa ajili ya kuzindua soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto ulioteketeza soko hilo mwaka jana. Makamu wa Rais amewasili mkoani Mbeya jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua Soko la Tunduma baada ya kukamilika kwa ukarabati kufuatia soko hilo kuungua moto mwaka jana.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment