HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 25, 2012

idara ya Afya simanjiro kufanya jitihada za kuboresha miundo mbinu

Na Mery Ayo,Arusha

IDARA ya afya wilayani Simanjiro imesema kuwa itafanya jitihada za kupata fedha ili kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu ambayo inaikabili idara hiyo hali ambayo itawafanya wakazi wa eneo hilo kupata huduma bora za kiafya.

Ambapo idara hiyo ya afya katika wilaya ya simanjiro inakabiliwa na changamoto mbali mbali za miundo mbinu hali ambayo inasababisha wakazi wa eneo hilo kutopata huduma nzuri za matibabu.

Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa wilaya ya simanjiro dr Kusirye Ukio wakati alipokuwa akiongea katika mkutano wa wadau wa watoa huduma za afya simanjiro uliofanyika mjini hapa wenye agenda ya kuchukua mpango kazi wa kila mdau kwa mwaka 2012 -2013.

Dr Ukio alisema kuwa katika idara hiyo ya afya ina upungufu wa asilimia 36 ya watumishi wa afya ikilinganishwa na eneo la utoaji wa huduma ambapo lina watu 1,095 waliopo kwenye ukubwa wa mraba 2591 ambapo watumishi waliopo hawatosholezi mahitaji halisi.

Aidha alisema kuwa miundo mbinu iliyopo katika idara hiyo ni michache ikiwa ni pamoja na nyumba za watumishi,huduma za afya za uzazi kwa akina mama na zahanti hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa miundo mbinu hiyo inaboreshwa mapema iwezekanvyo

."Hadi sasa hatua zimechukuliwa za kujenga nyumba ambapo nyumba nne tayari zimeshajengwa na kuanzia mwezi april mwaka huu kuna mpango wa kuhakikisha kuwa nyumba nyingine kumi za watumishi zitajengwa na wafadhili mkapa Foundation kupitia mradi wa global Found mzunguko wa tisa hii yote ni ili kuboresha huduma kwa wananchi"alisema Ukio.

Aidha katika mkutano huo pia una lengo la kuzuia mwingiliano wa kazi pamoja na kuhakikisha kuwa mpango kazi wa kila mdau unakuwa katika kitabu kimoja .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad