HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 25, 2012

MKUTANO WA KAMATI TENDAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA, WAANZA MJINI ARUSHA

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Mb) Mjini Arusha leo, mara alipofika nchini kuhudhuria Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa) unaofanyika mjini Arusha. Mhe. Rose Mukandabana ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika akiongoza kikao cha kamati tendaji ya chama hicho walipokutana mjini Arusha leo. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Mb) ambaye pia ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.
Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa) Dk. Thomas Kashililah ambaye pia ni katibu wa Bunge la Tanzania akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) (Kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi ya chama hicho iliyokutana Mjini Arusha, leo.
Wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa), wakiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho kilichofanyika mjini Arusha leo. Kutoka kushoto ni Mhe. Byabarumwanzi Francois, Mbunge kutoka Burundi, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Request Mutanga (Mb) Muweka Hazina wa CPA Afrika, na Mbunge kutoka Bunge Zambia na Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) Makamu wa Rais wa CPA Afrika na pia Spika wa Jimbo la Gauteng, nchini Afrika Kusini.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika akiongoza kikao cha kamati tendaji ya chama hicho walipokutana mjini Arusha leo. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Mb) ambaye pia ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.Picha na Owen Mwandumbya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad