
Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo bwana Masanja mkandamizaji, Stara thomas pamoja na mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi ya wimbo huo.
Baadhi ya mambo aliyoyafanya Mh. Mlata ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video hiyo.
Pia studio ya Pro arts ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari.
Wimbo huo umepongezwa na wengi, kwani ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na pia kitendo cha kuwakusanya waimbaji pamoja kimewabariki wengi.
Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Pia waimbaji wa nyimbo za injili nchini wameshauriwa kujiunga na chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita), Kuna faida nyingi sana za kujiunga na chama.
Fomu sasa zinapatikana kwa viongozi wa chama hicho. Kwa mawasiliano zaidi 0754 818767, 0716560094 au watembele www.johnshabani.blogspot.com
Mh.
Martha Mlata akiwa katika picha ya pamoja na Masanja Mkandamizaji na
waimbaji wengine wa muziki wa injili wakati wa kurekodi wimbo wao huo wa
miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment