Ujumbe wa Cuba ukiongozwa na Waziri wao wa Mambo ya Nje. Bw. Bruno Rodigues Parrilla ukifuatilia kwa makini zoezi la upigaji kura wa Azimio la kuitaka Marekani iondoe vikwazo vya kiuichumi dhidi ya Cuba
Zoezi
la Upigaji kura lilivyokuwa likiendelea ndani ya Ukumbi wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa hapo jana. pichani ni mashine ikionyesha namna kila
nchi ilivyolipigia kura Azimio la kuitaka Marekani ionde vikwazo vya
kiuchumi dhidi ya Cuba. Jana ilikuwa ni mara ya ishirini kwa azimio hilo
kupigiwa kura dani ya Baraza Kuu. jumla ya kula za ndiyo zilikuwa 186,
nchi 2 zilipiga hapana , na nchi tatu hazikupiga kukataa wala kukubali
azimio hilo kwa lugha ya Umoja wa Mataifa zili Abstein.
Na Mwandishi Maalum
New York
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa juzi ( jumanne ) kwa mara nyingine tena wamepitisha azimio la kuitaka Marekani iondoe vikwazo vya kiuchumi, biashara, uwekezaji na fedha dhidi ya Cuba.
Azimio hilo namba A/66/L.4 ambalo liliwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bw. Bruno Rodriquez Parrile. lilipitishwa kwa kupigiwa kura wakati wa mkutano wa siku moja wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa. Katika upigaji kura huo, nchi 186 zilipiga kura ya ndiyo, nchi mbili zilipiga kura ya hapana na nchi tatu hazikuegemea upande wowote.
Hii ilikuwa ni mara ya Ishirini mfululizo,kwa nchi wanachama kulipigia kura azimio hilo. Mwaka 1991 kwa mara ya kwanza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliamua kuingiza suala la vikwazo kwa Cuba katika ajenda.
Wajumbe 40 wote waliozungumza katika mkutano huo, walikuwa na m ujumbe mmoja tu. Nao ni wa kuitaka Marekani kuondoa vikwazo hivyo kwa kile kilichoelezwa kwamba kuendelea kuwapo kwake ni ukiukwaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa na sheria za kimataifa hususani zile zinazokataza nchi moja kuingilia mambo ya nchi nyigine.
Baadhi ya wasemaji walieleza kuwa, vikwazo hivyo vimeinyima fursa Cuba na raia wake ya kuendelea kiuchumi, kijamii na kibiashara. Lakini pia kunazinyima nchi nyingine haki zao za msingi za kuwekeza na kufanya biashara na Cuba.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Mohamed Hamza. Yeye alisema licha ya maazimio ya kupinga vikwazo dhidi ya Cuba kupitishwa kwa kura nyingi. Bado wananchi wa Cuba wanaendelea kuteseka kwa kuendelea kuwapo kwa vikwazo hiyo.
Akasema Tanzania inaamini vikwazo dhidi ya Cuba vinaweza kuondolewa wakati wowote na kwa haraka. Ikiwa nchi hizo mbili zinazopingana, ( Cuba na Marekani) zitaonyesha utashi wa kisiasa na kuamua kukaa mezani kumaliza tofauti zao.
Balozi Hamza akasema kwa vikwazo hivyo kuendelea kuwapo wanaoumia ni wananchi wa kawaida na ambao hawana hatia yoyote.
Akatoa mfao kwa kusema “ kule Tanzania ninakotoka tunamsemo wetu; ‘. wapiganapo fahari ziumiazo ni nyasi’. Kwa kweli wananchi wa Cuba wameshaumia vya kutosha. Tanzania tumepiga kura ya kuunga mkono azimio hili ili kuonyesha mshikamano wetu na wananchi wa Cuba.
Awali akiwasilisha Azimio hilo , Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bw. Bruno Rodriquez Parrile, alisema Marekani inafahamu wazi sababu za kuiwekea vikwazo nchi yake. Na kuwa sababu hiyo na kwa mujibu wa Waziri huyo ni kutaka kuiangusha serikali ya nchi yake.
Alisema kikwazo hivyo ni kuingilia masuala ya ndani ya Cuba na kutaka kuwaamulia hatma yao. Na kufafanua kwamba , mpaka sasa vikwazo hivyo vimeshasababisha hasara ya zaidi ya dola za kimarekani 975 bilioni.
Kama hiyo haitoshi Waziri Parrille aliongeza kuwa kutokana na vikwazo hivyo, nchi yake haiwezi kuingiza nchi humo bidhaa mbalimbali kutoka nje na wala yenyewe haiwezi kusafirisha nje ya nchi hiyo bidhaa inazozalisha.’
Kama hiyo haitoshi Waziri huyo amesema, vikwazo hivyo vimesababisha wananchi wengi kupoteza maisha na wengine wakiendelea kuteseka kwa kukosa dawa kama vile za kutibu kansa kwa kuwa dawa hivo zinatakuwa kuagizwa kule zinakotengenezwa na kupatikana yaani Marekani.
Aidha wazungumzaji wengine walibainisha kwamba, vikwazo hivyo vimeendelea kuiweka serikali ya Cuba na hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiriwa na mdodoro wa uchumi. Na kwamba kunahatari kubwa kwa nchi hiyo kutoweza kufikia Malengo ya Maendeleo ya Millennia (MDGs)
Kwa upande wake msemaji wa Marekani, Bw.Ronald Godard,yeye alieleza kuwa suala la vikwazo dhidi ya Cuba ni suala la mataifa hayo mawili. Na kwamba Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa halikupashwa kulijadili kwa kuwa si mahali pake.
Akaongeza kuwa ni Serikali ya Cuba yenyewe ndiyo inayowaletea matatizo wananchi wake wa kubinya demokrasi na haki za binadamu miongoni mwa mambo kadhaa.
Bw. Godard alidai kuwa serikali yake imejitahidi kulegeza baadhi ya masharti na kuruhusu misaada ya kibinadamu yakiwamo madawa na vyakula na uingizaji wa biadhaa za kilimo na mifugo. Aidha akasema Azimio hilo lilikuwa limeficha baadhi ya mambo na lilikuwa na mpango wakuzidi kuleta mkanganyiko dhidi ya wajumbe hao na jumuia ya kimataifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment