HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 26, 2011

Bryan Robson kuwasili kesho kwa ajili ya kambi ya Airtel Rising Stars

Bryan Robson
Mchezaji nyota wa zamani wa Klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Bryan Robson anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kufungua kliniki ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kliniki hiyo itaanza Jumapili, Oktoba 30 chini ya makocha wa Klabu ya Manchester United ambao ni Mark Fagan, Paul Bright na Billy Miller na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi za Kenya, Malawi, Sierra Leone na Tanzania.

Kliniki hiyo itakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars 2011 ambayo ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Andrew Cole, ambaye aliitumikia Klabu yake hiyo kwa misimu saba na kuisaidia kutwaa mataji matano kati ya 19 ambayo Manchester United imeyanyakua hadi sasa.

Airtel Rising Stars ni mpango kambambe wa kutafuta vipaji chipukizi vya soka kutoka ngazi ya chini hadi Taifa. Airtel Rising Stars ilishirikisha shule za sekondari 24 mwaka huu kutoka mikoa ya Mwanza, Iringa, Morogoro na Dar es Salaam ambapo washiriki walionyesha uwezo mkubwa wa soka na hasa katika fainali zake ambazo zilichezwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia juu ya michuano hiyo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Leodger Tenga alisema,’ Huu ni mpango muhimu sana kwa maendeleo ya mpira wa miguu hapa Tanzania. 

Na kile ambacho kinafanya Airtel Rising Stars kuwa muhimu zaidi ni ule ushirikiano wa kampuni hiyo na Manchester United, ambayo ni moja ya Klabu kubwa duniani. Hii inaifanya kuwa moja ya kitu kikubwa kutokea katika soka la Tanzania. Tunayofuraha kuwa kwenye ushirikiano huu na tunahaidi ushirikiano wetu zaidi ya hapo’.

Airtel inayofuraha kujihusisha na soka ambayo imekuwa ikiwaunganisha pamoja jamii pamoja na kuwafanya wachezaji kupata mbinu za soka ambazo zitawezesha waweze kuishi kwa kutegemea soka kama ajira.

Kliniki hii itawapa fursa vijana kupata mbinu mpya za soka chini ya wakufunzi bora zaidi na kuwafanya kuongeza uwezo zaidi.

Programu ya Airtel Rising Stars ni mpango wa Afrika nzima wenye lengo la kuwajengea mawakala, makocha, mamlaka za soka na wadau wengine fursa ya kuona vipaji vya wanasoka chipukizi na kutumia nafasi hiyo kuviendeleza ili kupata wachezaji wazuri kwa faida ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad