Watanzania
tunaoishi katika jiji la Atlanta na vitongoji vyake tumeshtushwa,
tumehuzunika na tumesikitishwa mno na taarifa za ajali ya meli ya Spice
Islander iliyotokea September 10 2011.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awalaze peponi wale wote waliofariki na tunawaombea wafiwa subra katika kipindi hiki kigumu.
Tunawashukuru sana wale wote waliofanya kazi ya kuokoa maisha na kusaidia kwa namna moja ama nyingine katika janga hili.
Halikadhalika,
tunamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kukatisha safari yake ya nje
ya nchi kwa ajili ya kushughulikia janga hili. Pia tunamshukuru Dr.
Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania
kuwa mstari wa mbele katika kuwafariji wafiwa.
Kwa
Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Kwanza
wa Rais Wa Zanzibar Maalim Seif, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wa Zanzibar, Inshallah mwenyezi
Mungu atawasaidia katika kuukabili mtihani huu.
Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajiun.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.
John Kazilo
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Waishio Atlanta
No comments:
Post a Comment