HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 11, 2011

Rambi rambi toka kwa Watanzania-Ugiriki


Vijana wa Kitanzania waishio Ugiriki wanatoa salam za rambi rambi kwa watanzania wote hususan wazanzibari wa mkoa wa nungwi kufuatia janga la kuzama kwa meli ya abiria.

Baada ya kuwapa Pole tunapenda kutoa masikitiko yetu kwa watanzania waliochukulia janga hili kama ni jambo jepesi tu,Ajali hii ilitokea mnamo majira ya sa tisa za usiku na habari zilianza kusambaa tokea wakati huo kupitia mitandao mbali mbali lakini cha kusikitisha ni kuwa hata televisheni ya taifa haikujali kabisa kufuatilia nakuwapa habari watanzania kwa ujumla.

Kampeni za uchaguzi huko ingunga zilianza bila kujali na kulikuwa na burudani za kutosha ikiwemo dansa na wachekeshaji,Kampuni ya simu za mkononi Vodacom iliendelea na shuhuli zake za uandaaji wa Miss.Tanzania bila kujali nini kimewasibu ndugu zetu wa Kizanzibari ambao ni watanzania kwa ujumla.

Nchi nyingi zilizoendelea huandaa nambari maalum za simu kupiga bure kwa waathirika au mwenye habari yoyote ya kusaidia kuokolewa miili au majeruhi,cha kushangaza kampuni hizo hazijajihusisha kabisa.

Ingekua ajali hii inatokea wakati mashindano ya miss Tanzania yanafanyika kusingekuwa na lawama lakini mashindano yalifanyika usiku baada ya masaa zaidi ya 14 kutokea ajali na kusambaa kwa kasi habari za ajali hizo.

Sifikiri nchi yoyote mfano UK wakiomboleza mabomu ya 7/7 ikawa Scotland wanacheza ngoma na London wanaomboleza!

Kwa kweli tumesikitishwa sana na vitendo hivi,hii inaonesha dharau kubwa kwa wawekezaji ambao wanajali maslahi yao tu na sio maslahi ya wanaowatumikia.

Tanzania ni taifa moja na sio kama vile shilingi moja yenye sehemu mbili mkia na kichwa,Janga linapotokea kote basi ni la kitaifa tu haijalishi limetokea sehemu gani.

Kwa kumalizia tunapenda kumpongeza Rais Kikwete kwa kukatisha ziara zake muhimu na kuweka kambi Zanzibar,vile vile pongezi kubwa kwa serikali ya Zanzibar kwa jitihada za uokoaji wa hali ya juu na pia wafanya biashara wenye vyombo vya usafiri kwa kujitolea bila kujali maslahi yao,Na pia Wananchi wa kijiji cha nungwi kwa kujitolea masaa 24 kuokoa na kupokea maiti na waliojeruhiwa.

Tunatoa salam nyingi sana kwa Rais Dr.Shein,Makamo wa kwanza na wa Pili wa rais,pia waziri wa nchi Mh Aboud kwa kuwa mstari wa mbele kushuhulikia janga hili na kuwa pamoja na wanachi kwa kipindi chote hiki.Tembelea website yetu kwa habari zaidi.http://www.tanzaniansingreece.org

Mungu ibariki Tanzania.

IT Manager
Abdul

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad