Afisi ya Mufti wa Zanzibar na Afisi ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuiya mbalimbali za Kidini Nchini, inawaalika Waislamu wote katika Kisomo maalum cha Kuwaombea Ndugu zetu wapenzi waliofariki katika Ajali ya kuzama kwa Meli ya "MV SPICE ISLANDERS" tarehe 10/09/2011, kitakachofanyika katika Uwanja wa Maisara siku ya Jumatatu tarehe 12/09/2011, baada ya Sala ya Alasiri.
Kabla ya Sala hiyo ya Alasiri patasaliwa sala Maalum ya "GHAAIBU" kwa kuwaombea ndugu zetu wote waliofariki katika Ajali hiyo.
Shime Waumini wote Wanaume kwa Wanawake tuhudhurie kwa Wingi na Kwa Wakati ili tuweze kuwahi Shughuli zote zilizopangwa kwa Ajili ya Kuwaombea ndugu zetu wapenzi.
Inapendeza kwa wote watakaohudhuria kuja na MISALA na si vibaya pia kuchukua MISAHAFU.
AHSANTENI.
F.S. Soraga
KATIBU WA MUFTI,
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment