Wazamiaji
12 kutoka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku wa kuamkia leo
mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya ulinzi na
usalama hapa nchini ili kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna mili
iliyokwama kwenye Meli ya MV Spice Islander iliyozama chini ya bahari
eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi wiki
iliyopita.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Aboud Mohammed, amesema
kuwa wazamiaji hao wamewasili wakiwa na zana za kisasa za uzamiaji na
kwamba kazi ya kwanza itakayofanywa na timu hiyo ni kuhakikisha kuwa
wanaifikia meli hiyo iliyozama umbali wa karibu nusu kimometa kwenye
mkondo mkubwa wa maji na majabali.
Bado
Serikali na wananchi mbalimbali wanadhani kuna miili ya watu waliokwama
katika vyumba vya meli hiyo tangu ilipozama usiku wa Jumamosi Septemba
10 mwaka huu ikiwa na idadi ya watu isiyojulikana.
Makundi
ya wananchi wamekuwa wakitaja idadi ya ndugu na jamaa waliosafiri na
Meli hiyo na ambao hawajapatikana wakiwa hai ama miili yao kiasi cha
kutia shaka kuwa huenda bado wamenasa ndani ya vyumba vya meli hiyo
iliyozama chini ya kina kirefu cha mkondo wa bahari ya Hindi.
Tangu
kuokolewa kwa abiria 619 na kuopolewa kwa miili ya watu 197 hadi jana
jioni, hakujapatikana mtu hai ama mwili wa abiria aliyekufa maji ukielea
juu ya maji ama kukokotwa kupelekwa mwambao mwa nchi kavu.
Katika
eneo ilipo Meli hiyo zipo Meli nyingine za MV Kasa ya Jeshi la Wananchi
wa Tanzania pamoja na MV Mamba ya Jeshi la Polisi ambazo zote
ziliwasili alfajiri siku iliyotokea tukio hilo la kuzam,a kwa MV Spice
Islander.
KIMSINGI AJARI YA MELI ZANZIBAR IMEGUSA HISIA ZA WENGI HASA WALE WALIO ONDOKEWA NA WAPENDWA WAO,NA MUNGU NAAMINI ATAWAPIGA KONDE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE.
ReplyDeleteSALAAM KWA WANA WAVUTI KIMSINGI NI JAMBO LA KUSIKITISHA SANA KWA WANANCHI PAMOJA NA WAKAZI WOTE WA JAMUHULI YA ZANZIBAR KWA AJARI HII ILIYO TOKEA, KIUKWELI AJARI HII IMEGUSA HISIA ZA WENGI ASA KWA WALE WALIO POTELEWA NA WAPENDWA WAO.NA TWENDELEE KUMUOMBA MUNGU ATUPE SUBILA NA NINAAMO\INI MWENYEZI ATAWAPIGA KONDE WALIOPOTELEWA NA NDUGU ZAO. PIA KWA VYOMBO VYA HABARI TUNAWASII WAENDELEE KUONYESHA WANANCHI HAMPAO KIMSINGI HAWAPO KATIKA ENEO LA TUKIO HABARI ZOTE ZINAZO ENDELEA NA HAO WAZIMIAJI WALIO TOKA AFRIKA YA KUSINI.
ReplyDeleteKwanza nawapa pole wafiwa na watanzania wote tupo pamoja katika msiba huu.Mimi nilifikiri kuwa serikali hii ya ccm ingekuwa imejifunza toka katika ile ajali ya mv bukoba kule kanda ya ziwa kwa kuweka sheria na utaratibu wa kudhibiti vyombo vibovu na kujaza kupita kiasi.Na hili suala la kusubiri wazamiaji toka afrika kusini mimi haliningii akilini hata kidogo,kama tuna jeshi la wanamaji na polisi wa kikosi cha maji kwanini mpaka leo hatuna kikosi maalum cha wazamiaji iwe toka jeshi la maji au polisi?nini faida ya kuwa na jeshi la maji na polisi wa kikosi cha maji kama kuzamia majini hadi tusubiri afrika kusini?mimi naona hakuna faidi;kwahiyo vunja ilo jeshi la maji na hicho kikosi cha maji cha polisi maana wanakula mishahara mikubwa ya bure!
ReplyDelete