Hapa ni Kijiji cha Lipupu Wilayanu Nanyumbu,Mkoani Mtwara ambapo nilikuwa siku za hivi karibuni kwa majukumu ya kikazi.na hii ikuwa ni safari ya kutoka kijijini hapo kuelekea Kijiji cha Mtalikachawa ambapo huu ndio usafiri wake.ni mwendo wa masaa mawili kwa Baiskeli kutokea katika hicho kijiji cha Lupupu.
Hapa nikiwa nimezungukwa na watoto wanaoishi kwenye Kijiji cha Lipupu,Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wakiangalia picha niliyokuwa nimewapiga kwa kutumia Kamera hiyo niliyoshika.
Mtaalamu wa utegaji wa mboga rasmi katika kijiji cha Mtalikachawa mkoa Mtwara akimezea mate mshkaki wa panya a.k.a mboga rasmi a.k.a Samaki nchanga kama aliokuwa akituonyesha
Kazi na Dawa,baada ya kupiga kazi iliyonipeleka huko nikajikuta nimefika hapa na kuanza kula Mihogo iliyokuwa inamenywa na kukatwa katwa tayari kwa kuanikwa ili baadae ile kusagwa na kuwa unga wa kupikia ugali.
Wakati wa kurudi nilikula mueleka na Baiskeli nikiyokuwa nikiitumia na ndio hapo hapo nikapata na kupumzika maana nikikuwa hoi ile mbaya.
Mnyororo wa Baiskeli nao ukaanza kuleta za kulena,nikaona isiwe tabu maana mambo mengine sio mpaka upeleke kwa fundi Juma akutengenezee,nikaamua kuonyesha ujuzi wangu menyewe na safari ikaendelea kama kawaida.
No comments:
Post a Comment