HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 17, 2011

HITILAFU YA UMEME NDIO KILIKUWA CHANZO CHA MOTO ULIOTEKETEZA SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA


Moto bado unaendelea kuwaka taratibu huku watoto wakiokota mabaki ya bidhaa mbali mbali zilizoungua na moto katika soko hilo.
Mabaki ya majiko ya mkaa na vigae vyake.
"kufa kufaana" Vibaka wakitoka na vyuma chakavu katika banda la sido lililoungua kwa moto.
Soko limebakia kiwanja tu,hakuna kilicho salia, pia umati wa watu wakitazama soko baada ya kuungua kwa moto jioni hii.
Jengo la sido mbeya nalo limeteketea kwa moto.
Haya ni mabaki ya mabati na vyuma vilivyoteketea kwa moto.

NA MWANDISHI WETU KUTOKA ENEO LA TUKIO.

ASUBUHI YA JANA TAREHE 16.09.2011 NCHI IMEINGIA KATIKA JANGA LINGINE AMBAPO SOKO KUU AMBALO NI JIPYA LA SIDO MWANJELWA MKOANI MBEYA LILITEKETEA KWA MOTO MAJIRA YA SAA 3:50 ASUBUHI, MOTO HUO AMBAO ULIWAKA KWA MUDA WA MASAA MAWILI BILA KUZIMIKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA KUPOTEZA MALI ZA WATU WENGI. 

IKIWA NI MIAKA MICHACHE TUU KUPITA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUPATA PIGO KUBWA BAADA YA SOKO KUU LA MWANJELWA KUUNGUA MOTO NA KUWALAZIMU WAANZE UPYA BIASHARA ZAO KATIKA SOKO HILO LA SIDO AMBALO NALO NDIO LIMEWAKA MOTO JANA.

HABARI ZAIDI ZINASEMA BAADA YA MOTO HUO KUANZA,ILICHUKUA MASAA MAWILI MPAKA MAGARI YA ZIMA MOTO KUFIKA NA KUANZA KAZI YA KUSAIDIA KUZIMA MOTO HUO AMBAPO WALIKUWA WAMECHELEWA HIVYO KUZIDI KUSABABISHA UPOTEVU WA MALI ZA WENYE MADUKA.

JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA PAMOJA NA MIGAMBO WALIKUA KATIKA ENEO HILO KUHAKIKISHA USALAMA UNAKUWEPO WA KUTOSHA,KUTOKANA NA KUWA NA VIBAKA WENGI AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUIBA MALI ZA WANANCHI.

KATIKA TUKIO HILO LA MOTO KUCHOMA SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA BAADHI YA MAMBO YALITOKEA IKIWA NI PAMOJA NA MTU MMOJA KUGONGWA NA GARI ALIPO KUWA ANAJARIBU KWENDA KUOKOA MALI ZA WAFANYA BIASHARA HAO, PIA KULIKUWA KUNA MFANYA BIASHARA ALIKUA ANAZUIA DUKA LAKE ILI WEZI WASIIBE KATIKA DUKA LAKE NA KUUNGUA KWA MOTO, INAHOFIWA HUYO NDIE MTU PEKEE AMEPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO HILO. 

PIA INARIPOTIWA KUWA KUNA MAMA MJAMZITO AMBAE ALIPATWA NA UCHUNGU NA KUTAKA KUJIFUNGUA KATIKA ENEO LA TUKIO LAKINI WASAMALIA WEMA WALIMWOKOA NA KUJIFUNGUA SALAMA.

WANANCHI WASIO NA MEMA AMBAO WAKATI JESHI LA POLISI LIKIWA LIKIJARIBU KUWASAIDIA WATU, WANANCHI HAO WALIANZA KUPIGA MAWE MAGARI HAYO YA POLISI NA PIA KUWATUPIA MAWE POLISI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO KUANGALIA HALI YA USALAMA,HATA HIVYO POLISI HAO WALIFANIKIWA KUWASHINDA BAADA YA KUWATUPIA MABOMU YA MACHOZI.

AKIZUNGUMZA NA MMOJA WA WAFANYA BIASHARA KATIKA SOKO HILO ALIEJITAMBULISHA KWA JINA LA GODEN MWAKALINGA ALIELEZA KUWA CHANZO CHA MOTO HUO KILITOKANA NA HITILAFU YA UMEME KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA BWANA MMOJA ALITAMBULIKA KWA JINA LA KHALIFA NA KUSABABISHA MOTO HUO KUWAKA NA MPAKA KUPELEKEA KUTOKEA KWA HASARA HIYO KUBWA KATIKA SOKO HILO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad