Wana chadema
tuliopo jijini Turini nchini Italia Tunaungana na watanzania wenzetu
woote kuhudhunika kwa janga/msiba mkubwa ulio likumba taifa letu. Ndugu
watanzania ni msiba mzito kwani tumepoteza wazazi weetu naam mama zeetu,
baba zeetu, kaka zeetu , dada zeetu na wadogo zeetu Eh Mungu wa Rehema
uwarehem milele amina.
Tunatoa
pole kwa wale woote walioguswa kwa njia moja au nyingine na hili janga
kubwa duniani. Tunatoa pole kwa serikali ya nchi yeetu iliyopo
madarakani. watanzania poleni saaana.
Kwa
kuzuia majanga ya aina hii kwa mda ujao , tunaiomba serikali kuimarisha
ukaguzi wa vyombo vya usafiri sio tu baharini bali pia na nchi kavu na
anga ili kupunguza majanga ya aina hii. Mungu ni mwema , tukiweka
mikakati madhubuti tutafanikiwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WAPE UIMARA NA NGUVU KUPITA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WALE WOOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.
AMEN!!!
No comments:
Post a Comment