HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 12, 2011

ATCL yashusha Ndege mpya Dar tayari kuanza kazi upya


Never say never with ATCL
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Paul Chizi (mwenye suti) akiipokea ndege hiyo

Ndege ya aina ya Dash 8-300 ya Shirika la Ndege la Tanzania  (ATCL) iliyokuwa nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu kwa matengenezo  imerudi  nchini juzi jumamosi jioni tayari kuanza kazi.

Ndege hiyo iliyokuwa inaendeshwa na Kapteni Pandya na Kapteni Lila iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere saa 12.45 jioni na kupokewa na wafanyakzai wa ATCL wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Paul Chizi.

Akiongea na vyombo vya habari uwanjani hapo Bw. Chizi alisema Shirika lake linajipanga kumaliza taratibu muhimu kabla ya kuanza tena safari zake. Alisema iwapo mambo yote yatakuwa yamekamilika kufikia tarehe 25 Septemba mwaka huu, ndege hiyo itaanza safari za kwenda moja kwa moja Kigoma kila siku.

Aliongeza kuwa baada ya  muda mfupi, wataanza safari za kwenda Tabora mara nne kwa wiki. Bw. Chizi ambaye ameteuliwa hivi majuzi kuongoza ATCL alisema baada ya mwezi mmoja wataanza safari za kwenda Zanzibar na Arusha.

Kuhusu kuongeza idadi ya ndege, Bw. Chizi alisema kuna Dash 8-300 nyingine ambayo itafanyiwa matengenezo hapa hapa nchini hivi karibuni ili kuokoa pesa na muda. Hata hivyo alifafanua kuwa tayari wameweka mkataba na kampuni ya Jetlink (T) Ltd wa kupata ndege nyingine haraka iwezekanvyo endapo kutakuwa na haja hiyo.

Bw. Chizi aliongeza kuwa  ATCL ina mipango ya muda mrefu ya kununua ndege zingine mbili za aina ya CRJ 700 zenye uwezo wa kubeba watu 70 ili kuzidi kuonggeza ubora wa huduma zake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad