HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 18, 2011

Moto wateketeza soko lingine jijini Mbeya usiku wa kuamkia leo

Usiku wa kuamkia leo huko jijini Mbeya,Moto ambao haukufahamika chanzo chake uliteketeza soko dogo lililopo maeneo ya Forest ya zamani karibu na Chuo kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria matawi ya Jijini Mbeya na kusababisha mabada kadhaa kuteketea kwa moto ambao uliwahiwa na kikosi cha zima moto cha mkoa wa Mbeya.
Mdau alietuletea picha hizi ambaye alifika eneo la tukio mapema leo asubuhi na kukuta moto umefanikiwa kuzimwa katika vibanda hivyo vilivyokuwepo sokoni hapo na kutuletea taswira hizi za mabaki ya mabanda yaliyoungua moto katika soko hilo yakiendelea kufuka moshi.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mjini,Bw. Evans Balama ambaye alifika katika eneo hilo la tukio usiku huo na kusaidiana na wananchi kadhaa waliokuwepo karibu na eneo la tukio kwa kujaribu kutaka kuokoa baadhi ya mali zilizokuwemo sokoni humo kwa kuuzima Moto huo kabla ya kikosi cha zima moto kufika eneo la tukio lakini hawakufanikiwa.
Mashuhuda waliokuwepo maeneo ya jirani na soko hilo walisema Moto huo ulianza majira ya saa 9:00 kamili usiku na muda si mrefu taarifa ziliwafikia kikosi cha Zimamoto na wao walifika eneo la tukio dakika 10 baadae na kufanikiwa kuuzima moto huo bila hata ya maigizo yao ya kila siku ya kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji au kuharibika kwa gari wakati wakiwa kwenye tukio.maswali mengi sana yamekuwa yakiulizwa hivi sasa Jijini Mbeya juu ya majanga ya moto katika masoko ya Mbeya kila siku na kwanini tahadhari hazichukuliwi mapema na wakati hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara??.Picha na Latest News TZ

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad