HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 18, 2011

Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mwanalibene Mroki Mroki

Mroki Mroki a.k.a Father Kidevu.
Leo naadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwangu. Nilizaliwa siku ya Jumatatu tarehe kama ya leo 18/9, kipekee namshukuru Mungu kwawema na rehema zake hadi naifika hii siku ya leo. 

Niwengi huenda nilizaliwanao siku moja na saa moja mwaka huo lakini leo hawapo, na wengine labda ni nyuma yangu. 

SINA CHA KUKUPA EE MUNGU WANGU ZAIDI YA SHUKRANI, SIFA NA UTUKUFU.

Hakika wazazi peke yao wasingeweza kunifikisha hapa nilipo leo bila ninyi, Ndugu, Jamaa na Marafiki. 

Namshukuru sana mama kwa kuniokota kisimani enzi zile na kunilea. (Yes watoto zamani tulikuwatunaokotwa mtoni au kisimani) pia namshukuru Mke wangu aliyepokea kijiti cha malezi miaka 4 iliyopita hakika ananilea vyema. 

Hivyo sina mengi sana ya kusema zaidi ya kusema Mungu awabariki sana. 

Mroki Mroki "Father Kidevu"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad