Vodacom Tanzania inapenda kuwashukuru
sana watanzania wote na hasa wateja wetu kwa kuendelea kushirikiana
nasi hadi hivi sasa tumefikisha wateja milioni 10.
Tuna kila sababu ya kuendelea kuwashukuru
wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kwa uaminifu na mchango wao
mkubwa wanaoendelea kuuonyesha kwetu kwa kipindi chote cha miaka 11
sasa.
Mafanikio mbalimbali tuliyoyapata hadi
hivi sasa ni matokeo ya kuelewa mahitaji muhimu ya wateja wetu na kuhakikisha
kuwa tunayatimiza na kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia huduma
zetu.
Kama tulivyowaahidi wakati wa mabadiliko
ya muonekano wetu, tunapenda kuwasisitizia kuwa tutaendelea kuyatimiza
yale yote tuliyowaahidi na kuyaboresha zaidi.
Vilevile, tunawahakikishieni kuwa tutaendelea
kuwa mtandao ulio bora na unaotoa huduma na bidhaa za bei nafuu zaidi
hapa nchini.
Ripoti ya idadi ya wateja kama
ilivyotolewa na TCRA
Mtandao | Vodacom | Airtel | Tigo | Zantel | TTCL | Sasatel | Benson |
Wateja | 10,000,000 | 5,927,417 | 4,671,263 | 1,354,098 | 226,153 | 8,498 | 2,074 |
Ahsante Tanzania.
Vodacom, kazi ni kwako
No comments:
Post a Comment