HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 16, 2011

Mkutano wa kuwachangia wahanga wa ajali ya meli Zanzibar, Copenhagen

Asalaam alaykum 

Tarehe 10, septemba 2011 ni siku ya majonzi makubwa kwa Zanzibar. Tarehe hiyo imetutia majonzi na simanzi nyoyoni mwetu. Mamia ya Wazanzibari wamepoteza roho katika ajali ya meli ya MV Spice Islander.

Kati ya waliopoteza roho zao ni watoto wachanga, watoto wa skuli, maharusi na watu wazima. Ni kwa masikitiko makubwa tunatanabahi kwamba mayatima wengi, wajane na wakongwe wengi wamepoteza watu waliokuwa wakiwa tegemea. 

Sasa maisha yao yamekabiliwa na upungufu wa matumaini. Kwa hivyo ni wajibu wetu kuwathibishia mayatima, wajane na wazee waliopoteza wapenzi wao kwamba tuko pamoja nao na kwamba nasi tulio Denmark na Skandinavia kwa jumla tunaungana na wenzetu Ulimwenguni kote hususan Zanzibar kuhakikisha kwamba majonzi ni yetu sote na sisi vile vile tutajaribu kuweka plasta kwenye jaraha lao zito. 

Kwa hvyo tunatangaza kwamba Jumapili ya tarehe 18 septemba, 2011 kutafanywa mkutano wa kukusanya misaada ya kuwapunguzia shida mayatima, wajane, wazee na waathirika wote kwa jumla. Mkutano utafanyika Tjørnegade 9, 2200 Nørrebro (nyuma ya makaburi ya Nørrebro), kuanzia saa 14:00 hadi 19:00. 

Wote mnakaribishwa. 
Wasalaam 
Dt. Yussuf

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad