
Na Sunday Shomari.
Bondia wa Tanzania Rodgers Mtagwa Alhamisi hii alijikuta tena akishindwa kupata nafasi ya kuitwa bingwa wa dunia baada ya refa kusimamisha pambano katika raundi ya pili dhidi ya bondia wa Mexico na bingwa wa WBC wa uzito wa unyoya Jhonny Gonzalez aliyetetea vyema mkanda wake.
Hii ni mara ya tatu mfululizo ambapo Rodgers Mtagwa anashindwa katika mapambano ya ubingwa ambayo ni nafasi nyeti sana kupata katika ndondi hapa Marekani hasa ukiwa umepoteza pambano lilikutangulia.
Kama nilivyoeleza katika andiko lililopita lazima Mtagwa atakuwa na Meneja mzuri na inabidi atumie nafasi hiyo vyema kwani amempa kila nafasi ya kuweza kuchukua mkanda wa dunia na ameshindwa mwenyewe.
Lakini pia nilieleza Mtagwa aliporwa ushindi New York Madison Square Garden dhidi ya Juan Manuel Lopez nafasi ambayo ingempatia ubingwa wa WBO na hilo liliwakasirisha wengi New York waliojaa kwenye uwanja ule.
Kwa hiyo pengine ingekuwa bora kwa meneja kuomba marudiano badala ya kupambana na bondia hatari wa Cuba Gamboa, sasa kwa wakati huu nafasi ya Mtagwa kuendelea kufikia hapa huenda ikawa mashakani lakini hatujui tutafanya juhudi ya kumpata yeye na meneja wake tusikie yapi waliyonayo.
No comments:
Post a Comment