baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo wakiingia katika Bandari ya Dar es Salaam jana kuanza safari yao kuelekea Zanzibar.
NA MWANDISHI WETU
KUNDI
jipya la taarab lijulikanalo kama T Moto Modern Taarab (T Moto),
limeondoka jijini Dar es Salaam jana Jumanne kwenda Zanzibar kwa ajili
ya kuanza kambi maalum kujiandaa na utambulisho wao.
Utambulisho
wa bendi hiyo inayomilikiwa na Amin Salmin ambaye ni mtoto wa Rais
Mstaafu wa Zanzibar,Salmin Amour (Komandoo) unatarajiwa kufanyika
Septemba 30, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandishi wa gazti hili, akiwa bandarini jijini jana alipokuwa
akiwasindikiza wasanii wa kundi hilo, Amini, alisema kuwa anaamini
baada ya vijana wake kurejea Dar es Salaam wakitoka huko,watakuwa
wameiva vilivyo kutoa upinzani wa nguvu kwa makundi mengine.
“Vijana
wangu ndio wanaondoka kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi ya kujinoa
hasa, naamini watakaporejea, watakuwa wameiva kiasi cha kuwawezesha
kutoa upinzani wa hali ya juu kwa makundi yanayojiita makongwe katika
muziki wa taarab,” alisema Amini.
Kwa
upande wake, kiongozi wa kundi hilo, Jumanne Ulaya (Vidole vya
Biashara) ambaye alikuwa ndiyo injini ya kundi la Jahazi Modern Taarab,
alisema: “Tunakwenda Zanzibar kujipanga vizuri tutakapotoka huko,tuweze
kutoa upinzani wa kweli kwa makundi mengine,Na pia tumejipanga kuweza
kuonyesha uwezo zaidi wa kuandaa muziki huu na hasa ukizingatia kundi
letu hili jipya linatumia magita matatu ili kuongeza radha ya muziki,
tofauti na makundi mengine yanayotumia magita mawili pekee.
“Tushatoa nyimbo mbili ni nzuri ambazo tayari zimeshatutangaza, tunakwenda kuongezea nyingine zenye ubora zaidi.”
Aidha
alisema kuwa tayari kuna nyimbo nyingine walizoanza kuzifanyia mazoezi
Dar es Salaam, hivyo wanakwenda kuanza kambi kwa lengo la kuziandaa kwa
umakini zaidi na kuzimalizia ili waweze kurekodi mapema na kuwapa raha
mashabiki wa muziki huo.
Juu
ya wanamuziki wake, alisema: “Jeshi langu limekamilika, nina wasanii
wenye vipaji vya hali ya juu ambao wengi wao ni wazoefu waliotoka katika
makundi mbalimbali yanayotamba kwa sasa katika muziki huu wa taarab.”
Aliyataka
makundi yote ya taarab kujipanga hasa kwani ujio wa kundi lao
linalojiita ‘Real Madrid’ kutokana na kunasa nyota kutoka makundi kadhaa
ya taarab, si wa kitoto, kutokana na kujipanga na mashambulizi ya kila
aina.
“Ninaye Bi Mwanahawa, huyu wimbo wake nimemuandalia mzuri tu, pia tuna Joha wimbo wake ndiyo tumesharekodi wa kwanza.
Jembe
langu jingine ni Mrisho Rajab ambaye yeye atatoka na wimbo wa Mchimba
Kaburi Sasa Zamu Yake Imefika, pia tuna nyimbo nyingine kama Aliyeniumba
Hajakosea na nyinginezo,” alisema.
Kuhusiana
na uamuzi wao wa kwenda kujichimbia Zanzibar, alisema: “Tunaenda
Zanzibar tuweze kukaa pamoja tofauti na hapa (Dar es Salaam) kila mmoja
anakaa kwake hivyo inakuwa vigumu kukusanyana kwa wakati mmoja na kuweza
kufanya mazoezi ya ‘Siriasi’.”
Miongoni
mwa waimbaji wa kundi hilo, Mosi Suleiman aliyetokea Dar Modern Taarab,
aliwataka wapenzi wa taarab kukaa mkao wa kula kwani hawaendi Zanzibar
kuuza sura bali ni kujifua hasa ili waweze kuyasambaratisha makundi
mengine yote ya muziki huo.
Hassan
Ally aliyetokea New Zanzibar Modern Taarab, aliwataka waimbaji wa
taarab, wakiwamo Mzee Yusuph wa Jahazi na Babu Ayoub wajipange upya
kwani kundi lao la T Moto si mchezo.
“Babu
Ayoub na wengine wakae sawa, nimejipanga kufanya mambo makubwa katika
taarab nikiwa na kundi langu jipya la T Moto ambalo litakuwa moto wa
kuotea mbali,” kama jina lake lilivyo, alijigamba Ally.
Mbali
ya Ulaya, Mosi na Ally, wasanii wengine walioondoka na kundi hilo
Jumanne ni Mrisho Rajab, Hasina Kassim, Fadhil Mnara, Rajab Kondo, Mussa
Mipango, Moshi Mtambo, Ally Kabula, Khanifa, Asha Mashanja, Sabra,
Rahma na wengineo.
Bi
Mwanahawa, Omari Kisila na wasanii wengine chipukizi watatu, watakuwa
ni wenyeji wa wenzao hao kwani tayari walishatangulia mjini Unguja ili
kuweka mambo sawa, huku Joha Kassim akitarajiwa kuungana na wenzake leo
Jumatano.
No comments:
Post a Comment