Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) na pia aliyewahi kuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania Sten Rylander(kushoto) akiwa na Kamishna wa Fedha za Nje wa Tanzania,Ngosha Said Magonya (wa pili kushoto), Waziri Mkuu Mstaafu wa Mauritania Zeine Ould Zeidane (wa pili kushoto ) na Katibu Mtendaji wa ACBF Dkt Franniel Leautier (kulia) wakati wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika(ACBF) leo mjini Arusha.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha,Ngosha Said Magonya akitoa maoni kuhusu viashiria vya kimaendeleo vya Afrika kwenye Mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana ulianza leo mjini Arusha.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha,Ngosha Said Magonya akizindua mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo,leo mjini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) na pia aliyewahi kuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Sten Rylander (kushoto) akipongezwa na Kamishna wa Fedha za Nje wa Tanzania Ngosha Said Magonya (katikati) mara baada ya kutoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana ulianza leo mjini Arusha. Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Mauritania Zeine Ould Zeidane.
Profesa Samwel Wangwe (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha,Ngosha Said Magonya (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana ulianza leo mjini Arusha na utafunguliwa rasmi kesho na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa mkutano huo ulioanza leo mjini Arusha na unatarajiwa kufunguliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kesho.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha
RAIS
Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) mjini Arusha kesho.
Katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa na viongozi waandamizi wakiwemo Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali.
Akizindua
mkutano huo Waziri wa Fedha wa Tanzania Mustafa mkulo alisema kuwa
suala la ajira vijana katika Nchi za Afrika bado ni kikwazo hali
inayosababisha baadhi yao kujiajiri wenyewe na wengine kubuni biashara
mbalimbali na kukopa kwenye benki na taasisi mbalimbali ili kupata
maendeleo na kuinua uchumi.
Aidha
utafiti uliofanyika kwama 2006 nchini Tanzania umeonyesha kuwa
asilimia 53.7 ya idadi ya watu milioni 42 wapo kwenye ajira na asilimia
68 ni vijana kati ya miaka 15 hadi 35.
Hayo
yalisemwa jana na Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na
Uchumi kwaniaba ya Waziri wa Fedha,Mustafa Mkulo wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa ACBF unaofanyika kwa siku tatu
Jijini Arusha.
Alisema
ingawa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 68 ya vijana hao baadhi yao
wameajiriwa na wengine wamejiari wenyewe katika sekta mbalimbali ambazo
zinawasaidia kuinua uchumi pamoja na kuleta maendeleo nchini.
Aliongeza
kuwa kila nchi inamatatizo ya ajira lakini nchi za Afrika hususan
Tanzania zinajitahidi kupambana na umaskini licha ya vijana kukabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la ajira ambalo
husababisha baadhi ya vijana hao kujiajiri wenyewe kutokana na ajira
kuuwa ngumu.
Alisema
mkutano huo utawezesha magavana wa benki kutoka nchi za Afrika na Ulaya
kujadili changamoto mbalimbali za ukosefu wa ajira kwa vijana,kutoa
mawazo yao katika kuleta maendeleo kwa nchi zote pamoja na kuwaunganisha
watu katika masuala ya siasa na uchumi ili kuweza kuleta maendeleo .
Naye
Katibu Mtendaji wa ACBF Dk, Frannie Leautier alisema mkutano huo ni
mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania na magavana hao watajadili
changamoto za ajira kwa vijana Barani Afrika na hatua gani zichukuliwe
ili kukabiliana na changamoto hizo pamoja na kujadili taarifa ya
viashiria vya uwezo wa Afrika kuelekea mkutano wa Busan utakaofanyika
Korea Kusini Novemba 2011.
Alisema
mkutano huo wa Korea utajadili utaribu ,usimamizi na ufanisi wa misaada
pamoja na kubuni mbinu zitakazowawezesha vijana wanaojiajiri wenyewe
kupata masoko ndani na nje ya nchi .
No comments:
Post a Comment