HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 7, 2011

Vodacom yaendelea kudhamini mbio za mashua

Baadhi ya Washiriki wa Mbio za Mashua, Zijulikanazo kama TANZACAT wakianza Mbio hizo jana katika Ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Klabu ya Yatch jijini Dar es Salaam ambapo Mashindano hayo yanayochukua siku saba yanadhaminiwa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mmoja wa washiriki wa mbio za mashua zijulikanazo kama TANZANCAT Evelyne Geubbels (kulia) akieleza namna mbio hizo za ufunguzi zinazodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania zilivyofana katika Klabu ya Yatch jijini, kushoto ni mshiriki mwenzake Jerome Vant Pad Bosch.
Mshiriki wa Mbio za Mashua zijulikanazo kama TANZACAT, Belia Klaassen, aliyewahi kushiriki mbio hizo kwa miaka kumi nchini Tanzania akielezea namna anavyofurahia kushiriki mashindano hayo tena na jinsi yalivyoboreshwa zaidi jana jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus Zervos akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo zilizoshirikisha mataifa 16 na kuwashukuru wadhamini wakuu Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus Zervos (wa pili kulia)akiwa na baadhi ya washiriki wa mbio hizo mara baada ya ufunguzi wa mbio hizo jana jijini ambapo zitaendelea kwa muda wa siku saba na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad