Blogs katika nchi yetu
ya Tanzania pamoja na sehemu nyingi duniani zimekuwa kiungo muhimu sana katika
kuupasha umma habari. Alianza Michuzi kublog wakafuatia wengi na wengi wao
wakiwa waandishi waliobobea na wasiobobea katika Nyanja ya habari Tanzania.
Nimesukumwa kuandika
haya ya leo kutokana mwenendo wa bloggers wengi ambao kwa hakika unaelekea si
tu kutukanisha taaluma ya habari, bali pia kuvunja maadili ya uandishi wa
habari kwa ujumla. Blogs zina kusudi la kufikisha ujumbe kwa mtindo uleule
ambao websites nyingine za habari kama cnn.com, bbcworld.com, ippmedia n.k
zingefikisha ujumbe kwa jamii. Ni dhahiri kwamba kanuni na sheria za uandishi
wa habari zinapaswa kuzingatiwa na wanablogu pia.
Tanzania tuna blogs
nyingi ambazo zimepoteza mvuto hasa kwa sababu ya ama kuhamisha habari za
wenzao au kuingia mikataba na wenzao ambayo inafanya zisiwe na jipya zaidi ya
kuhamisha kila kitu kilichotolewa na wenzao. Imefika wakati ambao nadhani hata
bloga anaweza kurusha habari za siku nzima akiwa chumbani kwake kwani
teknolojia ya ‘copy & paste’ inamruhusu kufanya hivyo. Lakini ni kosa kubwa
kwani wasomaji hutegemea mhabarishaji aliyejitolea kutoa habari kwa umma ajishughulishe
kutafuta habari na sio kunakili mapicha na habari zilizoandikwa na bloga
mwingine…. HII INABOA!
Nimeona blogs nyingi
ziki post story na picha kwa namna ile ile kitu ambacho inaonyesha kabisa
kwamba habari zimehamishwa tu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Zamani wakati
naripoti kwenye magazeti tulikuwa tunaelekezwa na wahariri wetu kuandika habari
kutoka angle tofauti mara unapokutana na mwandishi mwenzio aliyetoka chombo
unachokifanyia kazi ili msiandike habari inayofanana. Siku hizi mambo hayako
hivyo, mtu mmoja anaweza kuandaa habari na kuzirusha kwenye blogs kubwa tano
tofauti…NI AIBU!
Nawasihi mabloga wa
bongo mjitahidi kuingia mtaani kutafuta habari na sio kukaa baa na kunakili tu
habari zilizotolewa na wenzenu. Itaongeza msisimko zaidi pale utakapofungua
blog ya Michuzi ukakuta ina picha ama habari tofauti na Mjengwa, au Michuzijr,
au Mtaa kwa Mtaa, au Hakingowi. Na hata habari zikifanana, basi ziwe na taste
tofauti. Ni dhahiri kwamba siku nyingine unakuta blogs zote zina kila kitu
kinachofanana hata kama kuna typos.
Changamoto nyingine
ninayopenda kuwagusia wanabloga hawa ni kuchangamkia breaking news. Kumekuwa na
umaskini wa kuripoti matukio ya dharura au matukio mengine muhimu kutokana na
kutohangaikia habari. Unaweza kukuta tukio lililotokea saa nane mchana linakuja
kuripotiwa na magazeti kesho yake asubuhi, na hata bloga mmoja akilidaka hilo
basi hiyo habari utaikuta kwenye blogs zote kwa staili ile ile ya mmoja! Na hii si sahihi kabisa maana hata
sponsors wenu wanategemea kuona page zimesheheni habari na matukio
yanayoendana na wakati. Hivyo nawasihi bloggers wetu mjishughulishe kupata habari.
Proofreading ama
kuhakiki mnacho post ni ufa mwingine ambao si tu unakera bali pia unatia aibu
kwa taaluma ya uandishi kwa ujumla. Imefikia mahali ambapo hata majina ya watu
au vielelezo muhimu hukosewa bila hata mabloga hawa kusahihisha, ni jambo la
aibu. Nisingetegemea kuona gazeti la mzalendo, nipashe, mwananchi nk zimetoa
habari kwenye front page au kurasa nyinginezo na kukosea spelling halafu
wakaendelea kwa mtindo huo bila kujirekebisha. Blogs zetu zinapaswa zifuate
utaratibu wa kuzipitia na kusahihisha habari zao kabla ya kuzirusha.
Otherwise napenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kwenda na wakati, kwani bila kujitolea kwenu
kuanzisha blogs tungekuwa tunapitwa na mambo mengi sana, lakini tunapaswa
kupashana pale tunapoona panahitaji marekebisho ili twende sambamba na kasi ya
dunia.
Mwandishi wa kujitegemea
Article na ushauri mzuri. Uliyosema kweli sometimes yanakera. Kwa mfano unaenda kwa Mjengwa, Michuzi na HakiNgowi unakuta habari ni zile zile. Mwisho mtu unaamua tuu kuchagua blog moja na kuitembelea hiyo tuu.
ReplyDeleteLakini kitu kingine cha muhimu kujua ni kwamba sio wanablog wote ni waandishi wa habari by profession. Pia sio blogu zote ni kwa ajili ya habari. Kwa hiyo ni muhimu kuepuka generalisation ya blogs kuwa ni za habari tuu. Kuna blogs out there zinaandika mambo yasiyohusiana na habari na zinaelimisha na kuburudisha sana.
Sometimes blogu za news huwa hata wanachoweka sio news. Wakati mwingine huwa najiuliza ni vingezo gani mnatumia kutenganisha kati ya news na non-news.