HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 9, 2011

Wabunge wachachamaa leo kuhusiana na mgomo wa wauza mafuta nchini

Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto (Chadema) akichangia kuhusu sula la matatizo ya mafuta yanayoendelea nchini hivi sasa,kwenye kikao cha Bunge leo ambapo ametaka serikali iwachukulie hatua wafanyabiashara watakaokuwa wakaidi kutii amri ya serikali kuhusu uuzaji wa nishati ya mafuta.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini,January Makamba akitoa hoja yake binafsi ya dharura kuhusu tatizo la mafuta ya petroli nchini na ameitaka serikali kutoa tamko rasmi jinsi ya kumaliza tatizo hili ambapo wananchi wengi nchini wanapata taabu kuhusu usafiri katika maeneo mbalimbali.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa akichangia hoja ya dharura ya suala la mafuta Bungeni leo.
Mbunge wa Same Mashariki,Anne Kilango Malecela akichangia leo Bungeni kuhusu tatizo la suala la mafuta,kutokana na hoja ya dharura aliyoitoa Bungeni leo Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba kuhusu tatizo la mafuta nchini.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) pamoja na Naibu wake Ali Malima (kulia) wakiteta ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami (kushoto) akiteta na Naibu Waziri wake Lazro Nyalandu kabla ya kusoma Bajeti ya Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 leo Bungeni Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakiunga mkono hoja ya dharura alioyoitoa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba kuhusu tatizi la mafuta nchini.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad