HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 1, 2011

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA RASMI MAONYESHO YA 35 YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJINI DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharibu Bilal akifungua rasmi maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam leo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais, Dkt Mohamed Gharibu Bilal akizundua rasmi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam.
Msemaji wa Wizara ya Fedha,Ingiahedi Mduma akipokea kikombe cha ushindi wa kwanza leo jijini Dar es salaam kutoka kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt.Mohamed Gharibu Bilal baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la huduma za uchapishaji / uchapaji , na viandikia vya uelimishaji (Publishing ,Printing, Stationaries Exhibitors) wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya Dar es salaam yaliyofunguliwa leo jijini Dar es salam.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Mohamed Gharibu Bilal akiongoza viongozi wengine kuimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Raslimali watu Issa Nchasi( mweye suti nyeusi) wakifurahi ushindi wa kwanza wa watoaji wa huduma ya uchapishaji na viandikia vya uelimishaji kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es alaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad