Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ramadhan Khalfani (kushoto) akijadilina na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Meck Sadiq (kulia) kwenye viwanja vya maonyesho ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kutembele mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Meck Sadiq (kulia) akisalimiana na mbunifu wa mavazi kutoka Ghana,bibi Delight Forkuoh (kushoto) kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati Mkuu huyo alitembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiq (wa pili kushoto) akiangalia masharti kwenye banda la mbunifu wa mavazi hayo ambaye ni raia wa Ghana,Bi. Delight Forkuoh (kushoto) kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.Wengine Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Ramadhan Khalfan( wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara,Masha Hussein(kulia).
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza maelezo ya utengenezaji wa masharti kutoka kwa mbunifu wa mavazi hayo ambaye ni raia wa Ghana,Bi. Delight Forkuoh (kulia kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.Picha na MAELOZO,Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment