Warembo wa Vodacom Miss Sinza wakifanya mazoezi.
Michezo walioshiriki warembo hao, ilikuwa ni soka, ‘rede’, kukimbia pamoja na kuogeleaji, ambapo walionyesha umahiri mkubwa, huku wakishuhudiwa na wakufunzi wao, Amisuu na Salma Ali, pamoja na mwalimu wa shoo, Omari Musa ‘Bokilo’. Wakizungumza wakati wa tukio hilo, warembo hao walionyesha kufurahia michezo hiyo, wakiwapongeza waandaaji kwa hilo.
Akizungumza wakati wa nichezo hiyo, mwandaaji wa shindano hilo, Titina Makutikaalisema kuwa wameamua kufanya tukio hilo, ili kuanza kuangalia uelekeo wa warembo wao katika suala la michezo ambalo ni moja ya kipengele kinachoshindaniwa katika fainali za Dunia, Miss World.
Alisema kuwa pia mazoezi hayo, yalilenga katika kuwajenga zaidi warembo hao waweze kuwa wepesi katika kufuata na kushiriki katika maandalizi ya kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kuwa cha aina yake.“Warembo wetu bado wanaendelea na maandalizi yanayofanyika katika ukumbi wa Vatican kila siku ambapo maendeleo yameonekana kuwa mazuri hali inayotupa matumaini ya shoo yetu kuwa ya aina yake, alisema.
Alisema kuwa kutokana na ubora wa warembo wao, wanaamini taji la Miss Kinondoni litatua Sinza, kabla ya baadaye mmoja wa warembo wao kufanya kweli katika fainali za Miss Tanzania kuwania taji linaloshikiliwa na Genevieve Emmanuel kutoka Temeke.

No comments:
Post a Comment