HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 14, 2011

TBL YAKABIDHI MIKWANJA KWA TIMU ZA YANGA NA SIMBA LEO

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati wa kukabidhi hundi kwa timu za Yanga na Simba.wengine pichani toka kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe,Katibu Mkuu wa Yanga,Mwesingwa Selestine pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kabulu’.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja (kulia) akikabidhi mfano wa hundi kwa Katibu Mkuu wa Yanga,Mwesingwa Selestine.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja (kulia) akikabidhi mfano wa hundi kwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kabulu’.
Picha ya Pamoja.

Na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Wadhamini wakuu wa vilabu vya Simba na Yanga kampuni ya bia Tanzania (TBL)Kupitia bia yake Kilimanjaro Premium Lager leo imekabidhi hundi zenye thamani ya sh Milioni 40 kwa vilabu hivyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba wake.

Yanga ambao ndio mabingwa wa msimu uliomalizika wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilipata kitita cha sh. milioni 25 na Simba iliyoshika nafasi ya pili ilipata hundi yenye thamani y ash milioni 15.

Akiongea katika ofisi za TBL jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, David Minja alisema kuwa ‘baada ya kumalizika kwa msimu wa 2010/2011 wa ligi ya soka nchini, sasa wakati wa kutimiza ahadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili wa ligi Kuu.

‘TBL ingependa kutoa shukrani za dhati kwa Chama cha mchezo wa Soka nchini TFF, timu zote zilizoshiriki pamoja na viongozi na wanachama wao kwa ushirikiano wa hali ya juu waliouonyesha tangu kuanza kwa ligi mpaka mwisho wa msimu’.

Aidha Minja alisema kuwa TBL itaendelea kuwa mdhamini wa vilabu hivi vikongwe vyenye mashabiki wengi zaidi hapa nchini na kuwapa motisha wachezaji na viongozi ili waweze kujituma zaidi na kushinda vikombe na kuipa heshima nchi yetu katika ngazi za kimataifa.

Katika msimu uliopita wa ligi wa 2009/2010, timu ya Simba iliibuka bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kujinyakulia kitita cha sh milioni 25 kutoka TBL na timu ya Yanga Yanga ilishika nafasi ya pili ikajinyakulia kitita cha sh. milioni 15.

Viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga walihudhulia makabidhiano hayo ya hundi hizo kwa upande wa Simba makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kabulu’ alisema kuwa fedha hizo zitasaidia katika kuchangia maendeleo ya klabu hiyo inayojiwinda na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhindi ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kongo.

Katibu Mkuu wa Yanga,Mwesingwa Selestine alisema kuwa udhamini wa kampuni hiyo umekuwa chachu ya kufanya vizuri katika Ligi na hatimaye kuwa mabingwa kwa msimu uliomalizika, aliitaka kampuni hiyo kuongeza udhamini wake ili vilabu vingine ili kuleta msisimko na ushindani wa kweli katika ligi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad