HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU 3 YA WANAWAKE WAJASILIAMALI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mgulani jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiliamali yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko huo. Mama Anna Mkapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiliamali, yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko huo. Mama Anna Mkapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mshauri wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Robi Matiko wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mgulani jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo ya siku tatu ya Wanawake wajasiliamali, yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo. Mwinda Kiula.
Mmoja kati ya washiriki ambaye pia ni mjasiliamali wa katika Mafunzo hayo, Alya Riyami (aliesimama kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya ufunguzi huo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad