Msanii Joh Makini ambaye ni mmoja wa wasanii walioshinda tuzo la Kili za Muziki Tanzania 2011, akionesha umahiri wake wakati wa shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo hizo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma hivi karibuni.Ziara hiyo ya kuwashukuru wapenzi wa muziki waliowapigia kura imefanikishwa na wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii wa The Orijino Komedi, Mpoki akiimba wimbo wa shangazi katika shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo za Kili za Muziki Tanzania 2011,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma hivi karibuni.Ziara hiyo imefanikishwa na wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii mteule Juma Mataluma 'Nonya' akitawala jukwaa alipokuwa akitumbuiza wakati wa shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda Kili za Muziki Tanzania 2011,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma hivi karibuni.Ziara hiyo ya kuwashukuru wapenzi wa muziki waliowapigia kura imefanikishwa na wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Bendi ya Mapacha Watatu ambao ni miongoni mwa washindi wa tuzo za Kili za Muziki Tanzania 2011, wakilishambulia jukwaa wake wakati wa shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo hizo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma hivi karibuni.Ziara hiyo ya kuwashukuru wapenzi wa muziki waliowapigia kura imefanikishwa na wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Baadhi ya mashabiki wakishangilia kwa furaha wakati Msanii mteule Mwasiti akifanya vitu vyake katika shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo za Kili mwaka huu, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma hivi karibuni.Picha na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment