
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimbini iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kuweka jiwe la Msingi katika shule hiyo leo Mei 18, akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimbini iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akiwaaga baada ya kuweka jiwe la Msingi katika shule hiyo leo Mei 18, akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.

Wanafunzi wa Kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kangani iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, Siti Said Ali (kushoto) na Feda Ali Othman, wakiimba utenzi wenye ujumbe ikiwa ni sehemu ya burudani wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika Shule ya Msingi Mjimbini kuweka jiwe la Msingi leo Mei 18.
Wasanii wa Kikundi cha ngoma Mjimbini, wakiimba na kucheza miondoko ya Dahra, wakati wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika shule ya msingi Mjimbini mkoa wa Kusini Pemba kuweka Jiwe la msingi, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali leo Mei 18.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimbini, wakishangilia kufurahia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika shuleni hapo kuweka jiwe la msingi, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali leo Mei 18. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment