HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 6, 2011

UMOJA WA ULAYA NCHINI WAZINDUA WIKI YA ULAYA 2011 KWA WANAOJITOLEA KATIKA HUDUMA MBALI MBALI

Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania, Tim Clarke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuzinduliwa kwa ratiba ya sherehe za Wiki ya Umoja wa Ulaya zilizopangwa kufanyika katika maeneo mbali mbali nchini. Kushoto kwake ni Meneja wa Programu wa Jane Goodall Institute/Roots&Culture, Nsaa-Iya Kihunrwa na kulia ni Sadaka Gardi wa Tanzania House of Talents ambayo ni taasisi itakazo shiriki katika sherehe hizo.

Leo, Umoja wa Ulaya umezindua ratiba ya shughuli mbali mbali kwa ajili ya kusherehekea kazi za watu wanaojitolea hapa Tanzania.

Jitolee: Leta Mabadiliko
Ratiba hii itaanza Jumamosi tarehe 7 Mei kwa ushiriki kamilifu wa wafanyakazi wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania na Watanzania wengine katika miradi miwili ya maendeleo ya kijamii wilayani Kinondoni, na itaendelea mpaka Jumatano terehe 11 Mei huko Zanzibar.

Ratiba kamili inaambatanishwa na taarifa hii kwa vyombo vya habari.
Kila mwaka Umoja wa Ulaya huwa unachagua kauli mbiu za kusherekea mwaka husika.Ujumbe wa miaka mingine iliyopita ulikuwa kwa ajili ya kuchochea mijadala baina ya tamaduni mbali mbali, ubunifu na ugunduzi, na kupambana na umaskini na ubaguzi katika jamii. Mwaka huu kauli mbiu iliyochaguliwa ni Kujitolea.

Shughuli za kipekee zimeandaliwa kwa juhudi za pamoja Tanzania nzima kwa ajili ya kumulika na kukuza uelewa juu ya shughuli mbali mbali za watu wanaojitolea-watu wanaojitolea kihuduma kwa ajili ya watu wengine. Shughuli hizi zinajumuisha kuwatafuta, kuwatambua na kusherehekea juhudi za Watanzania hawa, wengi wao wakiwa hawatambuliki au kuzungumziwa katika mijadala ya umma ambao wamezihudumia jamii zao katika maeneo yote, afya, elimu, mazingira na kadhalika. Na ambao wamefanya hivi bila kujitangaza, bila
malipo, bila kutambuliwa.

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania Balozi Tim Clarke alisema; "Kila mtu anaweza kuleta mabadiliko. Jitolee muda wako, jitolee nguvu na hari yako, jitolee ujuzi wako na maarifa. Kutoa haya yote kwa bure, kuwasaidia wengine-hapawezi kuwa na chanchu nyingine ya kuleta mabadiliko kama hii. Mwandishi mmoja, Mark Twain, alisema: Ukarimu ni lugha ambayo hata viziwi wanaweza kusikia na vipofu wanaweza kuiona.

Pia yupo mtu mwingine aliwahi kusema: 'Hamna mtu anayeweza kufanya yote lakini kila mtu anaweza kufanya jambo fulani'. Matukio ambayo tunazindua leo, yameandaliwa na watu mbali mbali na mashirika/taasisi ambazo zimejitolea bila ubinafsi maisha na rasilimali zao kwa ajili ya kuwasaidia wengine. 

Katika muda huu muafaka kwa Tanzania kihistoria ambapo wananchi wanaangalia mafanikio waliyopata katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru, tunadhani ni vyema na ni muafaka kwamba sisi katika Umoja wa Ulaya pia tusherehekee juhudi za wale waliojitolea kwa hali ya juu kwa ajili ya kuwasaidia wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad