HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2011

TBL YASHIDA TUZO YA KIWANDA BORA KWA AFYA NA USALAMA MAHALA PA KAZI

Meneja Usalama, Afya na Mazingira wa Kampuni ya Bia Tanzania,Renatus Nyanda (kushoto) akikabidhi kikombe pamoja na cheti cha ushindi wa Tuzo za Afya na Usalama makazini kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Editha Mushi.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Editha Mushi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushindi wa tuzo za Afya na Usalama makazini ulioyoipata Kampuni hiyo ya bia hapa nchini hivi karibuni.kushoto ni Meneja Usalama, Afya na Mazingira wa Kampuni ya Bia Tanzania,Renatus Nyanda
Meneja Usalama, Afya na Mazingira wa Kampuni ya Bia Tanzania,Renatus Nyanda akizungumza machache juu ya ushindi wao huo leo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Editha Mushi akiwa ameshika kikombe pamoja na cheti cha ushindi wa Tuzo za Afya na Usalama makazini ulioupata kampuni ya bia Tanzania.

Kampuni ya Bia Tanzania imeshinda tuzo ya kiwanda bora kwa Afya na Usalama mwaka 2011. Tuzo za Afya na Usalama makazini zilizokuwa zimeandaliwa na kutolewa na Mamlaka ya Afya na Usalama sehemu ya kazi iliyo chini za Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana.

Mashindano ya Tuzo hizi yalihitimishwa kitaifa mkoani Ruvuma, Songea mnamo tarehe 28/04/2011.

Kampuni ya bia Tanzania iliingia kwenye kinyang’anyiro hicho na kuibuka mshindi wa kitaifa katika kundi la viwanda na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali. Akiongea wakati wa mazungumzo mafupi na waandishi habari,Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Editha Mushi alisema “ viwanda vingi vya uzalishaji vilishiriki ili kushindania tuzo hii na kampuni ya Bia Tanzania ikaibuka mshidi. Ni furaha kubwa sana kwetu kushinda tuzo hii.

Ushindi huu unatokana juhudi na mipango mbalimbali iliyowekwa na kampuni kuanzia kwenye ngazi ya kampuni mama ya SABMiller hadi kufikia kwenye ngazi ya kampuni ya Bia Tanzania. Kampuni imewekeza kwenye Mifumo na mitambo maalumu inayohakikisha usalama wa wafanyakazi wanapokuwa kwenye maeneo yao ya kazi.”

Aliongeza, “juhudi zilizowekwa na kampuni ni chachu kubwa sana katika mafanikio haya. Tumeshiriki tuzo nyingi za afya na usalama, kwa mwaka jana tulipata nyota tano za ukaguzi wa usafi, usalama na uzalishaji wa bidhaa bora. Nyota hizi hutolewa na kuendeshwa na shirika la kimataifa lijulikanalo kama NOSA. Tuzo hizi zote zinaendelea kuwa chachu zaidi kwa uongozi na wafanyakazi wa kampuni ya bia Tanzania.”

Nae Meneja Usalama, Afya na Mazingira wa Kampuni ya Bia Tanzania bw. Renatus Nyanda alisema, “Hii ilikuwa mara yetu ya pili kushiriki katika mashindano haya yanayofanyika kwa ngazi ya taifa ni furaha yetu kubwa sana kushinda tuzo hizi. Kwa miaka yote tumekuwa tukishiriki katika mashindano na ukaguzi unaofanya na kampuni ya kimataifa ujulikanayo kama NOSA. Kufuatilia ukaguzi wa kila mwaka ilikuwa furaha yetu kubwa kupata nyota tano za usafi, Afya na usalama makazi.”

Aliongeza, kama meneja wa kitengo cha usalama, Afya na Mazingira nafurahi sana kuona tumeweza kuelewesha uongozi na hata wafanyakazi na kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anachukua jukumu la kujilinda mwenyewe na hata mwezio.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad