HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2011

DK BILAL AUNGURUMA ISTANBUL KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAENDELEO YA NCHI MASIKINI

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa, ulioanza jijini Istanbul Uturuki Mei 9, ukitarajiwa kumalizika mei 13 mwaka huu. Mkutano huo unahusu Maendeleo ya nchi masikini.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika chumba cha mkutano alipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu.
Makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Maalim, walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini, unaoendelea Jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Anna Tibaijuka, akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyihaji Makame (katikati) na Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndugule, wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano wakati walipohudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiingia kwenye Ukumbi wa Mkutano, wakati aliwasili kwenye ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi masikini Duniani. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu, jijini Istanbul Uturuki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo na Balozi mdogo wa Tanzania nchini Italia, Salvator Mbilinyi, wakati wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Istanbul, Uturuki walipo hudhuria katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi Maskini, ulioanza jana Mei 9, hadi Mei 13 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Msaidizi wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID), Donald K Steinberg (wapili kulia) na ujumbe wake wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofsnyika jijini Istanbul Uturuki kuhusu maendeleo ya Nchi Maskini Duniani. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo na Balozi mdogo wa Tanzania nchini Italia, Salvator Mbilinyi, wakati wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Istanbul, Uturuki walipohudhuria katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi Maskini, ulioanza jana Mei 9 na kumalizika Mei 13 mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Makamu wa Rais , Zahor Haji.Picha zote na Muhidin Sufiani wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad