HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2011

MWENYEKITI HALMASHAURI RUNGWE AUWAWA KWA KWA KUPIGWA RISASI

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja (pichani) ambaye ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku huu majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.

Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa alimiminiwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari ili kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.

Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa kwa ujumla.

Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri ripota wetu aliopo Rungwe atakavyokuwa anatuhabarisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad