HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2011

TAMASHA LA ZIFF LAZINDULIWA RASMI USIKU HUU KATIKA HOTELI YA MOVENPIC JIJINI DAR

Meneja wa Bia ya Tusker ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu (ZIFF),Rita Mchaki akizungumza usiku huu wakati wa uzinduzi ramsi wa Tamasha hilo litakaloanza kufanyika mapema mwezi ujao katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.Uzinduzi huu umefanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpic,jijini Dar.kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo,Marlene Larsson.
Meneja wa Tamasha la ZIFF,Daniel Nyalusi akizungumza muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa filamu ya siku nyingi ifahamikayo kwa jina la "HARUSI YA MARIAM" ambayo iliwapendeza wengi katika uzinduzi ramsi wa Tamasha la Filamu la ZIFF linalotarajiwa kuanza kuonyeshwa hivi karibuni katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.Uzinduzi huu umefanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpic,jijini Dar na kukutanisha wadau mbali mbali wa tasnia hiyo ya filamu.
Mkurugenzi wa ZIFF,Prof. Martin Mhando akiongea na wadau waliohudhulia uzinduzi huo usiku huu kwa kupitia mtandao jamii wa SKYPE na kutoa shukrani zake kwa waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea wakati wa uzinduzi huo.
Bendi ya THT ikitumbuiza usiku huu.
Hapa sijui ilikuwaje??maana hata mimi mwenyewe nshasahau.
Umakini ulitawala wakati Prof. Martin Mhando akizungumza na wadau kupitia mtandao jamii wa SKYPE.
Wadau wa Zantel pia walikuwepo.
Pozzz la picha.
Kila mtu alikuwa makini kusikiliza kila kilichokuwa kikizungumzwa katika uzinduzi huo.
Hata sie wadau wa Bwawa la Maini tulikuwepo katika uzinduzi huo.
Shadee na Dina Marios kutoka pande ya Clouds Fm pia walijumuika katika uzinduzi huo.
Wadau wakibadilishana mawazo.

Ambwene Yessaya a.k.a AY akiwa na Mdau Ahmed.
Wadau wa SBL pia walikuwepo,kati ni Meneja wa Bia ya Tusker,Rita Mchaku,kulia ni Bahati Singh na kushoto ni Ben Mariiki.
Warembo wakibofya.
Wageni waalikwa toka sehemu mbali mbali pia walikuwepo.
Wadau wa ZIFF.
Wadau wa SBL wakibadilishana mawazo.
Wadau wa Clouds TV wakiwakilisha ndani ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad