HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 9, 2011

MAMLAKA YA USIMAMAMIZI WA BIMA NCHINI YAFUNGUA OFISI KANDA YA KASKAZINI

Kamishna wa Bima Tanzania Ndugu Israel Kamuzora akiongea na wafanyabiashara ya bima (mameneja na maofisa waandamizi wa makampuni mbalimbali ya bima) mkoani Arusha ambapo alisisitiza umuhimu wa kufanyakazi kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi. Kamishna alisisitiza zaidi juu ya umuhimi wa kutoa huduma bora kwa wateja wa bima nchini.
Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima kanda ya Kaskazini Bibi Stella Rutaguza akifungua kikao cha wafanyabiashara wa bima (mameneja na maofisa waandamizi wa makampuni mbalimbali ya bima) mkoani Arusha hivi karibuni.

Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini imefungua ofisi kanda ya Kaskazini Jijini Arusha. Ofisi hii ya kanda ya kaskazini inajumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Tanga,Manyara na Arusha.

Akiongea na wadau wa Bima mkoani Arusha hivi karibuni, Kamishana wa Bima Tanzania Ndugu Israel Kamuzora,alieleza kuwa madhumuni ya kufungua ofisi hii ni kupeleka huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo karibu zaidi na wananchi.

Huduma zinazotolewa na ofisi hii ni kusajili makampuni,madalali na mawakala wa bima Nchini, kusajili wakadiriaji wa hasara wa mali na ajali (Insurance assessors and Loss adjusters), kufanya ukaguzi kwenye makampuni ya bima,kutoa elimu ya bima kwa umma na kusikiliza malalamiko ya wateja wa bima nchini.

wafanyabiashara wa bima mkoani Arusha wakimsikiliza Kamishana wa Bima Nchini Ndugu Israel Kamuzora alipokuwa akiongea nao kuhusu maswala mbalimbali yahusuyo biashara ya bima hapa Nchini.
Wafanyabiashara na Wafanyakazi wa Bima mkoani Arusha wakimsikiliza Mkuu wa kanda ya kaskazini Bibi Stella Rutaguza kwenye kikao kilichofanyika katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha hivi karibuni.
Wafanyakazi wa mamlaka ya Bima nchini kanda ya kaskazini (kutoka kushoto ni Ndugu Soud Sadique,Sigfrida Zacharia,Stella Rutaguza na Derick Owawa)
Wafanyabiashara wa Bima mkoani Arusha pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya Bima kanda ya kaskazini wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kikao chao katika hotel ya Kibopalace.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad