
Vimwana wanaoshiriki katika shindano la mwaka huu la Kimwana wa Twanga Pepeta, wanataraji kuunogesha usiku wa mwafrika unaofanyika kila siku ya Jumatano.
Vimwana hao ambao idadi yao imefikia 25 watawaonjesha kidogo mashabiki jinsi gani wanavyojua kunyonga kiuno huku wakipigiwa midundo mitamu ya African Stars Band “Twanga Pepeta” ambao huwa wanatoa burudani kali kila siku ya Jumatano katika Club Hiyo.
Utambulisho rasmi wa Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 ambao burudani yake itatolewa na Twanga Pepeta na Msanii aliyejitwa tuzo tano za kili music award za mwaka huu 20% unataraji kufanyika katika Club ya sun cirro iliyopo Sinza Ijumaa tarehe 06-05-2011. Fainali ya Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 iafanyika tarehe 03-06-2011.
MAIMARTHA JESSE.
MRATIBU WA SHINDANO.1
MAIMARTHA JESSE.
MRATIBU WA SHINDANO.1
No comments:
Post a Comment